This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Wednesday, March 5, 2014

CCM, Chadema, CUF wanavuruga Bunge, asema Dovutwa

Mjumbe wa bunge maalumu la katiba Fahmi Dovutwa akichangia mada wakati wa semina ya wajumbe hao ya kupitia vifungu vya rasimu ya kanuni juzi.Picha na Silvan Kiwale 
0


Dodoma. Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Fahmi Dovutwa alichafua hali ya hewa baada ya kuvituhumu vyama vya CCM, Chadema na CUF kuwa ndiyo vinavuruga Bunge kwa sababu ya misimamo yao.
Hali hiyo ilitokea wakati mjumbe huyo akichangia mjadala wa Rasimu ya Kanuni za Uendeshaji wa Bunge Maalumu la Katiba juzi.
Dovutwa alitoa shutuma hizo baada ya mjumbe mwingine, Julius Mtatiro kueleza kuwa amepitia Rasimu ya Kanuni lakini hakuona mahali panapoeleza mpangilio wa ukaaji wakati wa kupiga kura.
Hali hiyo ilimfanya Dovutwa, kusimama na kutoa tuhuma kuwa baadhi ya wajumbe wamehongwa na kwamba kuruhusu mpangilio maalumu ni kukaribisha mgawanyiko.
Alisema kukaa kwa mpangilio huo kutawapa nafasi viongozi mbalimbali kushinikiza wajumbe wao katika maamuzi ya mambo mbalimbali.
“Ukaaji wa sasa umezingatia masilahi ya nchi, utashi na matakwa ya wananchi. Watu wa CCM, CUF na Chadema ndiyo mnaharibu mkutano (Bunge),” alisema Dovutwa.
Dovutwa alisema vyama hivyo vinatofautiana katika masuala mbalimbali na misimamo yao ndiyo imetawala bunge hilo.
“Mnatulazimisha tuwasikilize nyie tu. Kwa hiyo Mwenyekiti usikubali, kikao hiki kizingatie masilahi mapana ya makundi mbalimbali,” aliongeza Dovutwa.
Baada ya kutamka hilo, mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kupitia Kanuni, Amon Mpanju alisimama na kumtaka Kificho kulisaidia Bunge hilo kwenda na utaratibu aliowatangazia juzi wajumbe, ambao wanatakiwa kuwasilisha hoja zao kwenye kamati kisha kutolewa uamuzi.
“Naomba uamuzi ukishafanyika, kiti chako kisiruhusu mtu mwingine kuingilia maana mchakato hautafika mwisho. Nawaomba wajumbe wenzangu tusilete michango inayoweza kuleta hisia za mgawanyiko miongoni mwetu,” alisema Mpanju.
Mtatiro alisema hakupendezwa na mchango wa Dovutwa na kutahadharisha ukweli hauwezi kukwepeka kwa kuwa kuna watu wanaotoka katika makundi mbalimbali.
“Wakati wa kupiga kura tunahitaji theluthi mbili ya wajumbe wa Tanzania Bara na idadi kama hiyo kwa wajumbe kutoka Zanzibar kwa hiyo ili kurahisisha kazi hiyo, wajumbe kutoka Zanzibar wakae upande wao na wale wa Bara wakae upande wao,” alisema Mtatiro.

Giza nene mabilioni ya IPTL, Tanesco


 Gavana wa BoT, Profesa Benno.PICHA|MAKTABA 

Dar es Salaam. Wakati haijafahamika nani aliyelipwa mabilioni ya shilingi yaliyokuwa kwenye akaunti ya Escrow katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kutokana na mvutano baina ya Tanesco na Kampuni ya IPTL, imebainika kuwa Bunge liliwahi kuagiza fedha hizo zisichukuliwe mpaka mitambo ya IPTL itakapokuwa chini ya Tanesco mwakani.
Hiyo imo katika taarifa ya iliyokuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2007.
Hata hivyo, Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alithibitisha jana kuchotwa kwa Dola za Marekani 122 Milioni (Sh195.2 bilioni) katika akaunti hiyo, lakini akakataa kutaja nani hasa aliyelipwa.
Mkataba wa miaka 20 baina ya IPTL na Tanesco ulisainiwa mwaka 1995 na ulitakiwa kuisha 2015 na mitambo hiyo kuwa mali ya Tanesco.
Hata hivyo, ukiwa umebaki mwaka mmoja kumalizika, imebainika kuwa mitambo hiyo imeuzwa kwa Kampuni ya Pan African Power, ambayo inatarajiwa kuingia mkataba mwingine na Tanesco ili iwauzie umeme.
Ndulu alisema fedha zilizokuwa kwenye akaunti hiyo ni Dola za Marekani 22 milioni na Sh161 bilioni za Tanzania ambazo zote kwa pamoja ndizo zilizofikisha jumla ya Sh195.2 bilioni.
Vyanzo vingine vilitoa takwimu mbili tofauti, kimoja kikisema kiasi cha fedha hizo kilifikia Dola za Marekani 270 milioni na kingine Dola 250 milioni. Kuhusu nani mwenye mamlaka ya kutoa fedha hizo, Profesa Ndulu alisema kwa mujibu wa mkataba wa kufunguliwa kwa akaunti ya fedha hizo, ni Wizara ya Nishati na Madini pamoja na IPTL.
“Hakuna mtu mwingine anayeweza kuidhinisha kutolewa kwa fedha hizo zaidi ya hao, kwa hiyo hao ndiyo waliosaini kutolewa kwa hizo fedha na taratibu zote zilifuatwa,” alisema Profesa Ndulu.
Alipoulizwa ni nani aliyelipwa fedha hizo, Profesa Ndulu alisema IPTL ndiyo iliyokuwa na mamlaka ya kusema ni nani alipwe na ilifanya hivyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alipoulizwa juu ya fedha hizo alisema: “Kwa kawaida huwa nina majibu mafupi sana, lakini kwa kuwa mmeamua kuandika uongo, endeleeni, siwezi kukujibu chochote wasiliana na hao IPTL wakujibu.”
Hata hivyo, haikuwa rahisi kumpata kiongozi wa IPTL kuzungumzia suala hilo kwa kuwa tayari kampuni hiyo ni mufilisi.
Msimamo wa Bunge

Sitta apiga jaramba kuongoza Bunge

Dodoma. Siku moja baada ya kuteuliwa na CCM kuwania uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema ameanza kupitia sheria na kanuni zitakazomwezesha kuliongoza huku akiahidi kutenda haki kwa wajumbe wote iwapo atachaguliwa.
Akizungumza mjini Dodoma jana, Sitta alisema: “Nawashukuru wote waliokuwa wakiniunga mkono na niseme wazi kuwa nitatenda haki kwa wajumbe wote wa Bunge Maalumu la Katiba.”
Alisema kazi kubwa aliyonayo baada ya uteuzi huo ni kuhakikisha kuwa anazipitia sheria na kanuni zinazoongoza bunge hilo na sheria nyingine kwa kuwa ndizo nyenzo zake za utendaji kazi.
Akizungumzia mchakato wa uteuzi ndani ya chama hicho na mchuano uliokuwapo kati yake na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge alisema: “Hii ni hatua ya awali na ya kawaida tu ndani ya CCM. Mara nyingi chama changu kikiona kuna mambo yanayoleta msuguano, basi huamua kuteua jina moja kwa ajili ya kugombea. Wameteua majina mawili kwa demokrasia kabisa. Ninakishukuru chama changu kwa kuniteua na kwa sasa najiandaa na uchaguzi.”
Suluhu: Nitafanya maajabu
Kwa upande wake, Mjumbe wa bunge hilo aliyeteuliwa na CCM kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Samia Suluhu Hassan aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba ana uwezo mkubwa wa kuliongoza Bunge Maalumu la Katiba na hana shaka katika uteuzi wake.
Samia ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), alijisifu akisema ana rekodi nzuri ambayo haitiliwi shaka kwa weledi wake na haoni tatizo kwa yeye kupewa nafasi hiyo.
“Nina rekodi nzuri ya kuongoza Serikali kwa muda mrefu na sijapata doa lolote, kwa hiyo sioni ugumu wowote,” alisema.
Samia aliwahi pia kuwa Waziri wa Ajira na Wanawake na baadaye, Waziri wa Utalii katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kabla ya kuwa Waziri wa Nchi, katika Ofisi ya Makamu wa Rais.
Kinana na mchakato
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alizungumzia mchakato uliompitisha Sitta kuwania nafasi hiyo na kusema ulilenga kuzuia mgawanyiko ndani ya chama.
Hata hivyo, alisema Chenge aliamua kwa hiari yake kujitoa baada ya kukubaliana na Sitta walipoitwa na uongozi wa chama kwa ushauri. Akizungumza katika mahojiano maalumu mjini Dodoma, Kinana alisema: “Kiutaratibu, yeyote ilimradi awe mjumbe wa Bunge la Katiba, angeweza kujitokeza kugombea uenyekiti. CCM, walijitokeza wawili walionyesha nia; Sitta na Chenge.

Tuesday, March 4, 2014

Tahadhari ya mvua kubwa

mvua_cdefe.png

Tafadhali pokea taarifa ya tahadhari ya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa Pwani 05 hadi 07/03/2014.
Na TMA (P.T)

Al-Shabab latangaza mauaji kupitia FacebookAl-Shabab latangaza mauaji kupitia Facebook

89BEEF09-6C9D-41F4-B935-D97E37371E73_w640_r1_s_4b322.jpg
Kundi la wanamgambo wa Somalia Al-Shabab limesema limeuwa watu watatu ambao linawashutumu kwa kufanya upelelezi katika mashirika ya kijasusi ya Marekani au Somalia. Kundi hilo lenye uhusiano na al- Qaida lilitangaza mauaji hayo Jumanne katika ukurasa wake wa Facebook.
Soma zaidi...

HIVI NDIVYO BILIONEA WA "UNGA" ALIVYODAKWA .... KUMBE NI KUNDI MOJA NA MTOTO WA LIYUMBA!!

BILIONEA maarufu jijini Dar es Salaam, Ali Khatibu Haji ‘Shkuba’(44) ambaye alikuwa akisakwa kwa muda mrefu na Kikosi Maalum cha Polisi Tanzania kwa madai ya kujihusisha na biashara haramu ya ‘unga’, amenaswa.
Bilionea Ali Khatibu Haji ‘Shkuba’(44) aliyenaswa na polisi.
Vyanzo vililiambia gazeti hili kwamba, mtuhumiwa huyo alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar, Februari 23, mwaka huu, saa sita mchana akijianda kwenda nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, mara baada ya Shkuba kukamatwa alisafirishwa usiku huohuo kwenda mkoani Lindi chini ya ulinzi mkali wa polisi ambapo Februari 27, mwaka huu aliunganishwa na watuhumiwa wengine na kufikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Kusini.
Madawa ya kulevya.

Shkuba ambaye ni mkazi wa Mikocheni, Dar ni mfanyabiashara mwenye maduka ya kubadili fedha (bureau de change) jijini, ana makampuni ya ulinzi na nyumba Mikocheni pia anamiliki magari ya kifahari likiwemo aina ya Jeep lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 150.
Vyanzo hivyo vilisema mtuhumiwa huyo alikuwa akisakwa na kikosi kazi tangu Januari 12, 2012 na inadaiwa kwamba alikimbilia nje ya nchi na kurudi kwa siri na ndipo jeshi hilo liliamua kumuwekea mtego.
Taarifa ziliendelea kusema kuwa, tangu vita ya kuididimiza biashara ya unga ianze nchini, hakuna bilionea aliyewahi kukamatwa zaidi ya mtuhumiwa huyo.
Gari aina ya Jeep lenye thamani ya zaidi ya milioni 150 ambalo ni mojawapo ya magari ya kifahari anayomiliki Shkuba.
Vyanzo vingine vya habari toka ndani ya jeshi hilo vinadai kwamba, Shkuba aliwahi kukamatwa mwaka 2006 kwa kuhusishwa na biashara hiyo haramu na kuwekewa ulinzi wa kifungo cha nje.
Habari zinadai kuwa, Januari 12, 2012, kikosi kazi cha kupambana na biashara hiyo kilipata taarifa ya kuwepo kwa madawa hayo aina ya heroin kiasi cha kilo 211 yenye thamani ya shilingi bilioni 9.4 mkoani Lindi yakiwa tayari kusafirishwa nje ya nchi.
Kikosi hicho kiliweka mtego maeneo ya Machinga Two mkoani humo na kufanikiwa kukamata unga huo uliokuwa umefichwa katika hoteli moja.
Binti wa Liyumba, Maureen Liyumba, siku alipokamatwa pamoja na wenzake wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 9.4 mkoani Lindi yakiwa tayari kusafirishwa nje ya nchi.
Watu wanne walikamatwa sanjari nao, akiwemo binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, Maureen Liyumba ambaye yuko mahabusu mpaka sasa na ameungana na Shkuba.
Vyanzo hivyo vilidai kwamba watu hao walikuwa wakiwasiliana na Shkuba ambaye watuhumiwa walimtaja na ndipo polisi walipoanza kumfuatilia.
Madawa ya kulevya aliyokamatwa nayo binti wa Liyumba na wenzake.
Siku moja nusura polisi wamkamate ambapo alikimbia na kulitelekeza gari lake aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T921 BPY ambalo bado linashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Lindi.
Inadaiwa kwamba polisi walipokwenda nyumbani kwake jijini Dar walimkosa na kila walipopiga simu zake zilikuwa hazipatikani hewani lakini baada ya kumkamata walimpeleka Lindi kwa helikopta.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa alipoulizwa juzi na Uwazi kuhusu madai hayo alithibitisha kukamatwa kwa Shkuba na kwamba tayari ameunganishwa na wenzake mkoani Lindi na wanaendelea kuwasaka mabilionea wengine ndani na nje ya nje ya nchi.

Maureen Liyumba pamoja na watuhumiwa wenzake.
“Ni kweli tulikuwa tukimsaka kwa muda mrefu Bwana Shkuba na tulijipanga vizuri sisi kikosi kazi hali iliyotufanya tumnase.
“Hii vita ya biashara haramu kwa sasa si kwa Tanzania tu bali ni vita ya dunia nzima, nawaomba wananchi wazidi kutupa ushirikiano na tutayafanyia kazi kwa siri maelezo yao,” alisema Kamanda Nzowa.

GPL

Taswira toka Bunge Maalum la katiba mjini Dodoma

 Wajumbe la Katiba Mhe. Sophia Simba (kushoto) akijadiliana jambo Mhe Janet Mbene pamoja na Profesa Ibrahim Lipumba
 Baadhi ya wabunge wakibadilishana mawazo kutoka kulia, Mhe. Jum Ali Khatibu, Mhe. Rashid Rai, Mhe. Kuga Mzirai na Mhe. Yusuf Manyanga
 Mhe.Ibrahimu Lipumba akichangia wakati wa semina ya kujadili rasimu ya kanuni za Bunge Maalum za mwaka 2014.
 Mwenyekiti wa bunge maalumu la katiba Mhe.Pandu Ameir Kificho (kushoto) akifurahia jambo na baadhi ya wabunge wa Bunge hilo kutoka Tanzania Visiwani.
 Mwenyekiti wa UPDP, Mhe. Fahami Dovutwa akijadiliana jambo na Mwenyekiti  wa TADEA Mhe. John Lifa Chipaka.
 Waziri mkuu Mhe.Mizengo Pinda akibadilishana mawazo na baadhi ya wajumbe wa Bunge maalumu la katiba baada ya kikao kuahirishwa 
 Mwenyekiti  wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe James Mbatia (aliyesimama) akiongea na Mwenyekiti wa chama cha TLP Mhe Augustino Lyatonga Mrema (aliyevaa kofia) semina ya kujadili rasimu ya kanuni zitakazo tumika wakati wa bunge maalum.
 Mhe.Peter Serukamba akichangia wakati wa semina ya kujadili kanuni za bunge la katiba mpya.
 Mhe Hawa Ghasia akichangia
 Mhe.Eng Christopher Chiza akijadiliana jambo na Mhe.Spika Anne Makinda.
 Mhe. Profesa Ibrahim Lipumba (kushoto)  akiteta jambo na Mhe. Profesa Mark Mwandosya wakati wa kujadili rasimu ya kanuni za Bunge.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Anne Makinda na Makamu wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Idd wakifuatilia kwa makini semina ya kujadili kanuni za Bunge.
 Mhe Stella Manyanya akichangia wakati wa Semina hiyo
Wajumbe Mhe Zakhia Meghji (kulia) na Mhe Hilda Ngoiye wakitoka nje wakati wa mapumziko. Picha zote na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kati